Dar/Bukoba.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limemwonya Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema, John Mnyika kutolihusisha na siasa, huku likikana
kuwanyang’anya kadi za kupigia kura maofisa wake ili kufanya hujuma
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Wakati
JWTZ likisema hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu
amesema suala hilo linapotoshwa na kuwa ni wajibu wa viongozi wa jeshi
hilo kuhakikisha askari wote wanatumia fursa ya kumchagua kiongozi wao.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Habari na Uhusiano kwa Umma,
Kanali Ngemela Lubinga alisema Jeshi limesikitishwa na kauli ya Mnyika
ya kwamba limewanyang’anya kadi za kupigia kura maofisa wake .
“Wanajeshi hawaruhusiwi kabisa kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa,” alisema Kanali Lubinga
Alisema Jeshi linaendelea na shughuli zake kama kawaida na halitaacha kukemea kauli za upotoshaji zinazolihusu jeshi hilo.
Awali,
Mnyika alisema Chama cha Chadema kimebaini uwapo wa mbinu za kutaka
kuhujumiwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu, kwani Serikali
imeviagiza vyombo vya usalama, kupeleka namba za vitambulisho vya askari
wote kwa wakuu wa vitengo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.CHANZO:MWANANCHI
IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON
Post a Comment