Kwa
mujibu wa chanzo cha ndani kutoka katika familia ya Diamond, Jumatatu
na Jumanne zilikuwa siku mbaya kwa Zari baada ya hali yake kuwa tete kwa
maumivu makali hali iliyoashiria kwamba, sekunde za kupata uchungu wa
kuzaa zilishafika.
SIKU ZA MATARAJIO
Taarifa
za awali zilidai kuwa, Jumamosi ya Agosti Mosi, mwaka huu ndiyo ilikuwa
siku ya makadirio ya Zari kujifungua lakini siku hiyo jua likachomoza
mpaka likazama, kukakucha. Siku ya pili ikaingia, Jumapili, ikafika
Jumatatu, Zari akiwa bado hajajaliwa kupata mtoto ndipo hali
ilipobadilika.
DIAMOND AMKIMBIZA HOSPITALI
“Hali
ilikuwa mbaya sana. Ikabidi Diamond amkimbize kliniki anayotumia Zari
iliyopo Masaki” kilisema chanzo hicho huku kikiomba hifadhi ya jina
lake.
DAKTARI ATIA NENO
Habari
zaidi zinadai kuwa, daktari wa Zari alimwambia Diamond kuwa, itabidi
mjamzito huyo akomalie mazoezi, hasa yale ya kujaza pumzi kifuani ili
aweze kujifungua kirahisi na ndivyo alivyofanya Zari.
HALI YAKE
“Ilibidi
Zari arudishwe nyumbani lakini hali yake kiafya ikiwa ya kusuasua kwani
hayuko kawaida. Si unajua wajawazito. Wakianza maumivu ya tumbo
(uchungu) wanakuwa kwenye mateso makubwa. Hali yake ni ya kumtazamia
sana.” Chanzo.
MAMA WA ZARI ATUA DAR
Habari
zilizolifikia gazeti hili Jumanne iliyopita zilisema kuwa, mama wa
Zari, Halima Hassan tayari yupo Dar nyumbani kwa Diamond baada ya hali
ya Zari kuwa tete.
“Mama
Zari ametua Dar tayari kwa dharura. Kaja tayari kwa kumsaidia mama
Diamond (Sanura Kasim) katika harakati za kuhakikisha mzazi huyo (Zari)
anahudumiwa sawasawa,” kiliongeza chanzo.
HOFU YA KUFICHA HABARI
Wakati
hayo yakiendelea, tayari kuna hofu kwamba, habari za Zari kujifungua
zinadaiwa haziwezi kuwafikia mashabiki moja kwa moja ili kumuepusha
mtoto na watu wabaya.
DIAMOND AZUNGUMZA
Paparazi lilipata nafasi ya kuzungumza na Diamond juzi ambapo aliulizwa kuhusu Zari kujifungua.
“Teh! Teh! Nyie watu kwa kutafuta habari bwana…Teh! Teh!”
KUHUSU USIRI
Diamond alisema hakuna usiri wowote wa Zari kujifungua kwani ni jambo la heri kabisa.
“Usiri wa nini sasa? Kwani kujifungua ni jambo baya? Mbona ni tukio jema tu. Hakuna usiri wowote ule,” alisema Diamond.


Post a Comment