Ziito Kabwe akiwa na mume wa Chiku Abwao na Chiku Abwao na kada wa ACT wazalendo. |
Zitto kabwe akiwa na wapambanaji |
Zitto kabwe akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini |
Chiku Abwao akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini |
Mgombe udiwani wa kata ya Mvinjeni Abuu Majeck akimpongeza mgombea ubunge jimbo la Iri nga mjini Chiku Abwao. |
KIONGOZI
wa chama cha ACT Wazalendo amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe (CCM) kuwa ni miongoni mwa wabunge wa mfano kutokana
na utendaji kazi wake mkubwa badala ya maneno bila vitendo.
Huku
aliyekuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa na mjumbe wa kamati
kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao akimtaka mbunge wa jimbo la Iringa
mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) kuwaeleza wakazi wa jimbo
hilo ndani ya miaka mitano ya ubunge wake amefanya nini zaidi ya
maandamano na kutukana watu .
Kauli
hiyo waliotoa wakati wa mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha
wagombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini na majimbo mengine ya mkoa
wa Iringa na kuwa siasa si maneno matupu siasa ni kazi zaidi ya
kuwakomboa wananchi waliokuamini katika maendeleo .
Alisema
Bw Kabwe kuwa mbali ya kuwa yeye ni ACT wazalendo ila hata
acha kuwazungumzia baadhi ya wabunge waliofanya kazi nzuri ya
kuwatumikia wananchi wao na miongoni mwa wabunge hao ni pamoja na
mbunge wa Ludewa Bw Filikunjombe kwani kazi aliyoifanya jimboni
inaonekana na kazi aliyoifanya ndani ya bunge katika kupigania
maendeleo ya wana Ludewa na Taifa kila mtazania anatambua mchango
wake .
Kwani
alisema kuwa kati ya manho makubwa ambayo Filikunjombe kama makamu
wake mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC)
kamati liyoifanya ni pamoja na kuhakikisha ripoti ya Escrow
inalindwa pasipo kuibiwa wakiwa wabunge watatu ambao walikesha
wakilinda ripoti hiyo isiibwe na mawaziri waliokuwa wakizingira
jengo walilokuwepo ili kuiba ripoti hiyo .
''
Siku ile tulikesha na mashuka yetu ya kimasai kuhakikisha ripoti
yetu haiibwi ili tuiingize bungeni na tukaiingiza bunge lakini
ile ripoti hadi leo kuna mambo hayajamalizwa kwani kampuni ya IPTL
ambao imenunuliwa na kampuni ya PAP ya Singa singa na kampuni hiyo
ya PAP hadi leo bado inapokea Tsh bilioni 4 kila mwezi kutoka Tanesco
hapo wazalishe ama wasizalishe'' alisema Kabwe
Alisema
kuwa kampuni hiyo asilimia 50 inamilikiwa na Seth Singa singa na
asilimia 50 nyingine zinamilikiwa na kampuni inaitwa simba Trust
iliyosajiliwa nje ya Tanzania na wamiliki wake hawafahamiki na
kuwa hizo ndizo hoja ambazo ACT wazalendo wamejiandaa kutembea nazo
katika kampeni ya uchaguzi mkuu .
Kabwe
alisema kuwa sakata ya ECROW bado halijaisha kwani bunge liliagiza
mtambo wa IPTL utaifishwe ila hadi leo bado kuna kigugumizi katika
kuchukua hatua juu ya suala hilo la kampuni ya kitapeli kuendelea
kulipwa mabilioni ya shilingi hivyo alisema kuwa haja ya chama cha
kati kuingia Ikulu ili kuweza kupambana na mafisadi wa Richimond
ambao leo wamejificha katika mwamvuli wa UKAWA .
Hivyo
alisema kuwa kila sababu wabunge kufanya kazi wanayotumwa na
wananchi wao kwa uadilifu badala ya kuwa wabunge wa maneno bila
vitendo na kuwa wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu ni vema
wananchi kuwapima wabunge wanaowachagua kwa kueleza wamefanya nini
majimboni badala ya kuwa na mbunge mpiga kelele zisizo za
kimaendeleo kwa wananchi wake .
Kwa
upande wake mgombea ubunge wa ACT wazalendo jimbo la Iringa
mjini Bi Abwao ambae amejiunga na chama hicho kutoka Chadema
alisema mbunge wa jimbo hilo mchungaji Msigwa ajiandae kukabidhi
jimbo hilo kwa ACT wazalendo kwani ameshindwa kuwatumikia wananchi
wa jimbo la Iringa mjini kazi waliyomtuma bungeni .
Alisema
kuwa kipindi cha miaka mitano ya mbunge mchungaji Msigwa jimboni
hapo hakuna jipya ambalo amelifanya zaidi ya maandamano na vurugu
ambazo wakazi wa Iringa mjini hawajapata kuziona na kuwa atazunguka
kila moja hadi nyingine kuwaeleza wananchi jinsi ambavyo mbunge
huyo alivyojaribu kuua nguvu ya vyama vya upinzani na kushindwa
kuwajibika kwa wananchi waliomchagua.
Post a Comment