Askari wa wanyamapori wakiwaadhibu raia katika Operesheni Tokomeza
MGOGORO
mpya umeibuka Ngorongoro baada ya Askari wa Wanyamapori wa Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro kudaiwa kuwapiga wafugaji wa kata za Endulen na
Alaitole wanaoishi pembezoni mwa hifadhi hiyo.
Chanzo
cha mgogoro huo kinaelezwa kusababishwa na baadhi ya wafugaji kupeleka
mifugo yao eneo la Mash ambalo hutumiwa kunywesha mifugo yao hasa
kipindi cha kiangazi, ambapo askari walipowakuta walianza kuwashambulia
kwa madai kuwa hawaruhusiwi kufuga mifugo yao katika eneo hilo.
Wafugaji
hao wameeleza kuwa katika kipindi hiki cha kiangazi ambacho wanakabiliwa
na uhaba wa maji hasa kwa ajili ya mifugo yao na wamekuwa na utaratibu
wa kutumia eneo hilo kwa makubaliano ya kila mwaka ila kwa mwaka huu
imekua tofauti kwani wamefukuzwa pamoja na kupigwa na askari hao kinyume
cha sheria.
Mzee wa
mila jamii ya Wamasai, Kadogo Olduati amesema kuwa kwa kipindi kirefu
wameishi katika ardhi mseto yenye mchanganyiko wa wanyamapori na mifugo
pamoja na binadamu bila kusababisha athari zozote katika kwa mazingira
na wanyama.
Olduati
ameitaka Mamlaka ya Ngorongoro isiegemee upande wa wanyamapori na
kuwasahau wafugaji ambao hutegemea ufugaji kuendesha maisha yao ya kila
siku.
Katibu wa
Baraza la Wafugaji, James Moringe ameiomba mamlaka ya Ngorongoro na
Baraza la wafugaji kwa pamoja kuitisha kikao cha haraka ili kuepusha
mgogoro huo ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na kuathiri
uhifadhi na utalii kwa ujumla.
Mhifadhi
wa Ngorongoro hakuweza kupatikana kuzungumzia tikio hilo kwa kuwa simu
yake ya mkononi haikupatikana, lakini pia walinzi waliwazuia waandishi
kuingia ofisini kwake mpaka watakapopata kibali maalum.
Post a Comment