UME ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), imekubali rufani 13 zilizokatwa na wagombea
ubunge katika majimbo mbalimbali nchini, huku majimbo 10 ambayo wagombea
wake walipita bila kupingwa, imewarejesha.
Kurudishwa
kwao kunafanya baadhi ya wabunge waliokuwa wamepita bila kupingwa, sasa
kuwa na wapinzani wao na baadhi ya majimbo hayo ni Bumbuli (January
Makamba), Peramiho (Jenista Mhagama), Ludewa (Deo Filikunjombe) na
Madaba (Mhagama), walitangazwa kupita bila kupingwa.
Hayo
yalibainishwa jana Dar es Salaam, na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC,
Kailima Kombwey wakati akitoa ufafanuzi wa pingamizi za wagombea ubunge
na udiwani, yaliyowasilishwa kwenye tume hiyo.
Akizungumzia
mapingamizi ya wabunge, Kasilima alisema walipokea pingamizi 56 za
wabunge wa majimbo mbalimbali na kati ya hayo, 32 yametolewa uamuzi,
huku wagombea 13 wakishinda rufaa hizo.
Majimbo
hayo na wagombea waliorudishwa ni kama inavyoonekana kwenye mabano,
Jimbo la Kinondoni, rufani mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo, Karama
Suleiman aliyewekewa pingamizi na mgombea wa CCM, Idd Azzan imekataliwa
na mgombea huyo amerudishwa kwenye kinyang’anyiro.
Post a Comment