MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, amedai kutishiwa amani baada ya kufanya maamuzi yake kisiasa ambapo amehamisha ushabiki wake kutoka CHADEMA na kwenda CCM.
Licha
ya mrembo huyo kudai kupokea vitisho mbalimbali, pia alidai amehama
chama hicho na kujiunga na CCM kutokana na kukubali sera za chama hicho.
“Sera
za chama nilichohamia zimenivutia na wala sikulazimishwa na mtu wala
sijapokea fedha wala gari kuhamia huko kama inavyosemekana, bali nafsi
na mapenzi pamoja na haki yangu ndiyo yaliyonipeleka huko.
“Nashangaa
maamuzi yawe yangu bado watu wanitumie jumbe za vitisho, mimi ni raia
kama walivyo wengine, umaarufu wangu usiwe sababu,” alisema Aunt, ambaye awali alikuwa akivaa magwanda CHADEMA
Post a Comment