Viongozi
wote wa CCM wa kata ya mkomazi na pamoja na wapiga kura 1,400 wa eneo
hilo wilayani Korogwe wamejiunga na CHADEMA huku baadhi yao wakiamua
kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwa tiketi ya chama hicho.
Wakizungumza
katika mkutano wa kampeni ulifanyika katika kijiji cha mikocheni
kilichopo kata ya mkomazi wilayani Korogwe baadhi ya viongozi hao pamoja
na wengine wa CCM katika kata sita waliokatwa majina yao katika zoezi
la kura za maoni kwa tiketi ya CCM wamesema wameamua kujiunga na
chadema pamoja na wapiga kura wao ili kuongeza nguvu kupata wawakilishi
wa wananchi katika baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya
Korogwe.
Kwa
upande wake katibu wa CHADEMA jimbo la Korogwe Bwana.Salim Sempoli
amemuomba mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la Korogwe
kuharakisha malalamiko ya wapiga katika baadhi ya vituo ambapo sehemu
kubwa ya majina ya wapiga kura katika jimbo la Korogwe vijijini
hayaonekani na hadi sasa hakuna utaratibu uliofanywa kusaidia tatizo
hilo kwa sababu linaweza kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani wakati
wa zoezi la kupiga kura.
Kufuatia
hatua hiyo mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema Emmanuel Kimea
amewataka wananchi kuwachagua viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya
taifa,ubunge na udiwani kwa sababu ndani9 ya chama kikoja changamoto
zinazowakabili katika kata ya mkomazi ikiwemo ya migogoro ya ardhi
haiwezi kumalizika kama hawatafanya mabadiliko.
Post a Comment