Mwanafunzi
wa Sekondary ya Loyola akipelekwa kwenye gari kuelekea Hospitali ya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo mchana, baada ya bajaj yenye namba
za usajili MC 402 AWD waliokuwa wameikodi na wenzake Bandarini wakitokea
Zanzibar kugongwa na Pickup Double Cabin yenye namba DFPA 826 katika
makutano ya barabara ya Sokoine na Azikiwe jirani na Benki ya NBC.
Katika ajali hiyo wanafuzi kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika
hospitali hiyo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakimfariji mwenzao Martha Silayo (katikati), aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.
Wananchi
wakiangalia bajaj iliyogongwa. Imeelezwa chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo mkali wa bajaj hiyo ambapo pia dereva wake alijeruhiwa.
Askari wa usalama barabarani na wananchi wakiwa eneo ilipotokea ajali hiyo.
Bajaj iliyogongwa ikiwa eneo ilipopatia ajali 'Kweli BOGOTI imegongwa'
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
Post a Comment