Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya Siku ya Wahandisi Tanzania mwaka
2015 Prof. Bakari Mwinyiwiwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu
Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini itakayofanyika Septemba 3 mpaka 4
jijini Dar es salaam.Kulia ni Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania
Muhandisi Steven Mlote na kushoto ni Msajili msaidizi wa Bodi ya Usajili
wa Wahandisi Tanzania (ERB) Muhandisi Benedict Mukama
Msajili wa
Wahandisi nchini Tanzania Muhandisi Steven Mlote (kulia) akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya
Wahandisi nchini yatakayofanyika Septemba 3 mpaka 4 mwaka huu.
Picha na Aron Msigwa-MAELEZO.
Na. Aron Msigwa - MAELEZO,1/9/2015.Dar es salaam.
KATIBU
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa
sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini Tanzania
itakayofanyika Septemba 3 hadi 4 jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya sherehe hiyo Prof.Bakari Mwinyiwiwa amesema Kuwa
Jumuiya ya Wahandisi nchini Tanzania inafanya maadhimisho hayo kwa mara
ya 13 toka kuzinduliwa kwake mwaka 2003 kuenzi mchango wa wahandisi
katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.
Kusna
Amesema
maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwawezesha waajiri na wahandisi
wazalendo na watumiaji wa huduma za kihandisi kutambua uwezo wa
wahandisi wazalendo na kampuni zao pia kuwahamasisha wanafunzi wa
kitanzania wanaosomea fani hiyo ili waweze kufanya vizuri katika masomo
yao.
Ameongeza
kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatajikita katika kuangalia masuala
mbalimbali ya maendeleo hasa ujenzi wa miundombinu,Maendeleo ya viwanda,
ukuzaji wa uwezo, na maendeleo ya shughuli za kilimo nchini Tanzani.
Kwa
upande wake Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Muhandisi Steven Mlote
ameeleza kuwa wakati wa maadhimisho hayo shughuli mbalimbali za
kitaaluma zitafanyika ikiwemo majadiliano ya kina kuhusu shughuli za
kihandisi nchini na miaka 15 ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025.
Amesema
wakati wa maadhimisho hayo kutakuwa na utambuzi na utoaji wa Tuzo na
zawadi mbalimbali kwa wahandisi na wahitimu wa Taasisi waliofanya
vizuri zaidi katika mitihani yao mwaka 2014/2015 pamoja na wahandisi
kurejea kiapo cha utii kwa taaluma yao.
Ameongeza
kuwa wakati wa maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho ya kiufundi ya
jumuiya za wahandisi wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Chuo
Kikuu cha Dar es salaam, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT),
Chuo Kikuu cha Uhandisi na Teknolojia St.Joseph na Chuo cha Ardhi (ARU).
Jumuiya
nyingine ni ile ya Makandarasi ,Kampuni za Ushauri wa
kihandisi,Mashirika na makampuni ya kibiashara na taasisi za utafiti.
Post a Comment