Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi nchini imefuta rufaa 38 za wagombea nafasi za
ubunge kati ya 54 zilizowasilishwa kupinga baadhi ya wagombea hao kwa
kuwatuhumu kutotimiza vigezo mbalimbali na kusema wagombea hao wanaweza
kuendelea na Kampeni majimboni mwao.
Kauli
hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa
Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhan kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Alisema
kuwa baada ya Wakurugenzi wanaoshughulikia uchaguzi kuzipitia
,waligundua kuwa rufaa hizo waliziona hazina mantiki na kukosa ushahidi
wa kutosha.
“Wagombea
waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa katika uchaguzi ni 16 na
Tume imewarudisha wagombea 13 kati ya hao na waliobaki watatu ,Tume
imeridhia maamuzi ya wasimamizi wa Uchaguzi”,alisema Bw.Ramadhani.
Aliongeza
kuwa Tume hiyo inaendelea kupitia rufaa za wabunge zilizobaki kwa
kushirikiana na wasimamizi wa uchaguzi ili kupata
vielelezo vinavyohusika na pindi itakapokamilisha zoezi hilo
itatoa taarifa yake ikiwa ni pamoja na rufaa 198 za madiwani kutoka
halimashauri mbalimbali nchini.
Aidha alisema
kuwa Tume hiyo itaendelea kusimamia haki na kufanya maamuzi ya
kuzingatia sheria kwa wagombea wa vyama vyote vilivyoshiriki katika
uchaguzi wa mwaka huu na kuwataka kuwa na imani na kazi inayofanywa na
Tume katika rufaa hizo.
Mbali
na hayo Mkurugenzi wa uchaguzi alisema kuwa Tume inatarajia kuanza
zoezi la uhakiki wa daftari la mpiga kura visiwani Zanzibar kuanzia
tarehe keshokuwa (03/09/2015) ambapo zoezi hilo litadumu kwa muda wa
siku saba.
Akiongelea
juu ya uhakiki wa taarifa za mpiga kura aliyejiandikisha alisema
unaweza kuhakiki taarifa zako kwa kupitia mtandao wa
tume www.nec.go.tz au kwa kupiga *152*00// katika simu na kupata
taarifa zote.
Post a Comment