CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kumshitaki mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli kwa madai ya kutumia vibaya nembo za chama hicho.
Ni
baada ya Dk. Magufuli kutangaza kuwa nembo ya Movement for Change (M4C)
ni Magufuli For Change wakati akifanya mkutano wake wa kampeni mkoani
Kigoma kwenye Uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji.
Katika mkutano huo Dk. Magufuli alisema “hawa jamaa zangu wa Chadema wananipenda, hata ile nembo yao ya M4C ni Magufuli for Change-maana yake Magufuli kwa Mabadiliko.”
Chadema
wanaratajia kufungua kesi hiyo Septemba 21 mwaka huu na kwamba, madai
hayo yatakwenda sambamba na madai ya kutumia kauli mbiu ya ‘mabadiliko Lowassa’ ambayo kaibadilisha na kuwa ‘mabadiliko Magufuli’.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ngome
Kawe, Mwanasheria wa Chadema, John Malya alisema “CCM imekuwa
ikivunja sheria za uchaguzi kila siku bila kuchukuliwa hatua yoyote na
mamlaka husika, wanatumia nembo za Chadema ambazo zimesajiliwa na
kujulikana.”
Hata
hivyo imeelezwa, baada ya Dk. Magufuli ‘kuiba’ alama hizo za Chadema;
wafuasi wake, bodi ya wadhamini na watu wake wa kampeni walianza
kusambaza mitandaoni nembo ya M4C huku wakidai ni nembo mpya ya CCM.
Malya
alisema mbali na hilo la kuiba nembo ya chama, wamekuwa na tabia ya
‘kukopi’ na ‘kupesti’ kila hatua inayo pigwa na Chadema na kuzitumia
katika kampeni zao.
Akivitaja
baadhi ya vitu vinavyokopiwa na CCM amesema, Magufuli amesikika mara
kadhaa akiwa anatumia sera na Ilani ya Chadema na Ukawa, pia amekuwa
akiiba kauli mbiu za Chadema pindi anapokuwa katika kampeni zake.
“Hii
ni dalili za kushindwa kwa CCM hana sera wameishiwa na ndio maana
wanafuata nyayo zetu kila tunapoenda na kila tunalofanya wanalifuatilia
na kuaza kutukopi. Kwa mfano sisi tunatumia Lowassa mabadiliko
mabadiliko Lowassa na wao wameshaiga kwa kutumia jina la Magufuli”.
Aidha,
Malya alisema Chadema inasikitushwa sana na kitendo cha Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kimya huku vitendo vya rushwa vinazidi
kukithiri toka kwa CCM.
Malya
alitaja baadhi ya matukio yenye viashiria vya rushwa kuwa, Magufuli
alionenekana akimpatia mtoto pesa taslimu elfu 30000 katika moja ya
kampeni zake, huku Mgombea mwenza wa CCM Samia Suluhu Hassani naye mara
kadhaa ameonekana akigawa pesa kwa wananchi wanaohudhulia katika kampeni
zake.
“Matukio
yote hayo bado tume imekaa kimya japo kuwa tumeshapeleka barua za
malalamiko na kutuahidi kulishughulikia kesho. Vivyo hivyo kwa Taasisi
ya Kushuhulikia Rushwa Tanzania (TAKUKURU) ambayo tulitegemea itakuwa ya
kwanza kukemea hilo lakini ipo kimya na tumeshaandika barua ya
malalmiko”.
Alidai,
pia CCM wamezidi kukiuka sheria za uchaguzi kwa kuyachana mabango ya
Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa hadharani na kwamba, wanakiuka
sheria
Alisema,
matendo hayo yote yanayofanywa na CCM yanakuika sheria za umiliki wa
nembo za biashara ya mwaka 1986 na kanuni ya umiliki huo ya 2000 pamoja
na taratibu zingine za umiliki.
Credit: Mwanahalisionline
Credit: Mwanahalisionline
Post a Comment