TETESI MPYA
Wakati
hayo yakijiri, habari kutoka chini ya kapeti zinasema kuwa mwigizaji
mwingine, Shamsa Ford naye anawindwa kutoka kundi la wasanii mashabiki
wa Ukawa, ambao wanafanya kampeni ili kumpa ushindi mgombea wao, Edward
Lowassa.
“Sijawahi kushawishiwa kutoka Ukawa, siwezi kutoka Ukawa, nitaendelea kuwa Ukawa kwa muda wangu wote,” alisema nyota huyo kuonesha kwamba naye ameshtuka!
“Sijawahi kushawishiwa kutoka Ukawa, siwezi kutoka Ukawa, nitaendelea kuwa Ukawa kwa muda wangu wote,” alisema nyota huyo kuonesha kwamba naye ameshtuka!
Lakini
katika mahojiano na gazeti hili wiki iliyopita, Nature alisema ni kweli
hivi sasa atafanya shoo katika kampeni za CCM, lakini akisisitiza kuwa
anafanya hivyo kwa kuwa yeye ni msanii na hiyo ni kazi yake.
Katika orodha hiyo pia yupo msanii wa filamu, Chuchu Hans ambaye awali alikuwa Chadema na Ukawa na kuvaa sare zao siku ya ufunguzi wa kampeni lakini siku chache baadaye aliamua kurudi CCM huku listi ikiongezwa na msanii wa vichekesho, Kitale.

HAWA WAMEJIPAMBANUA
Pia wapo wasanii ambao kwa muda wote wamejulikana kuwepo kambi moja wakiwa ni pamoja na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ (anadaiwa kuposti mitandaoni maneno ya kuwakaribisha Ray na Aunt kujiunga na CCM), Wema Sepetu, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ali Kiba, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Salome Urassa ‘Thea’, Davina ambaye jina lake halisi ni Halima Yahya na Rutta Bushoke ambao wanafahamika kuwa ni CCM damu.
Wasanii ambao wamejipambanua kuwepo Ukawa pamoja na wengine ni Jacqueline Wolper, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Husna Idd ‘Sajenti’, Haji Adam ‘Baba Haji’ na Kala Jeremiah, Jimmy Mafufu, Bob Junior, AT na Soggy Doggy
Post a Comment