Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimekemea kauli zenye kuwajengea hofu wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia unaoendelea kwa kutoa mifano isiyoshabihiana na hali iliyopo nchini ikiwemo kufananisha na nchi zenye machafuko
Katika
taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari imemtaka mgombea urais
kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mh. John Magufuli kufuta kauli zake
ikiwemo ya kufanisha mchakato wa uchaguzi na vuguvugu la mabadiliko ya
Libya pamoja na serikali yake kuwapiga risasi wahalifu wa kutumia
silaha.
Mh. Magufuli mnamo tar 28 Agost akiwahutubia wakazi wa Mbalizi Mbeya vijijini alisema “Msitoe
hukumu ya jumla zipo nchi zilifanya hivyo zilijuta,Libya ya Gadafi
ilikuwa ukioa unapewa nyumba, unatafutiwa mtaji ,elimu na umeme bure
lakini wananchi walichoka raha.....wakasema wanaondoka lakini wale
vijana waliosema wanataka raha na wale vijana waliosema wanataka
ukombozi wa haraka ndio wa kwanza kuvuka bahari ya Mediteranian kwenda
Ulaya."
Kituo
hicho kimesema kauli hizo zinatoa vitisho kwa wapiga kura kinyume na
demokrasia kwa kuwa huwezi kufananisha mabadiliko ya kimapinduzi ya
Libya na umwagaji damu uliotokea huko na mabadiliko ya amani kwa kupitia
mchakato wa uchaguzi za kidemokrasia.
Taarifa
hiyo imeogeza kuwa kauli hizo za mgombea huyo ni za kukemewa kwa
kuzingatia nchi na chaguzi zinaongozwa kikatiba na Katiba inakinzana
kabisa na kauli zilizotolewa na kiongozi huyo
Post a Comment