Mkuu
wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki (kulia) akiwa katika
bandari ya Dar es Salaam alipofanya ziara ya kujionea kuwasili kwa
Mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) tayari kuanza kwa
kuanza huduma ya kipindi cha mpito mwezi ujao. Kushoto ni Kaimu
Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga, wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni UDA Rapid Transit (UDA-RT),Bw. Robert Kisena
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wa pili
kushoto ni Msemaji wa Kampuni hiyo,Bw, Sabri Maburuki.
Sehemu
ya mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) yaliyowasili
katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya
usafiri katika kipindi cha mpito kwenye miundombino ya mfumo wa mabasi
yaendayo haraka (BRT)kuanzaia mwezi ujao
Mkuu
wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akijaribu basi la Mradi
wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar
es Salaam kujionea
kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa
huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha mpito
Mkuu
wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akishuka katika basi la
Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari
ya Dar es Salaam kujionea
kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa
huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mpito.
********
TATIZO
la usafiri katika jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua kufuatia
kuanza kupindi cha mpito cha mabasi Yaendayo Haraka (BRT) mwezi ujao
kufuatia kuwasili kwa mabasi 138 katika Bandari ya Dar es Salaam kutoa
China tayari kwa huduma ya usafiri.
Mkuu
wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki aliwaambia waandishi wa
habari jana wakati alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam
kujionea kuwasili kwa mabasi hayo, kuwa wakazi wa Dar es Salaama kwa
sasa wataanza kutumia usafiri wa mabasi hayo.
“Tumefikia
hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kwa
kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri
katika kipindi cha mpito," hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa
wakazi wa jiji hili", alisema na kuongezeas kuwa kampuni hiyo imepewa
jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili waweze kupata uzoefu na zabuni
ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu itakapo tangazwa itasaidia wao
kushindana.
Alisema
serikali ilifanya kazi kubwa kuwainganisha Kampuni ya Usafiri Dar es
Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya UDA-RT.
Aidha
alikanusha kuwa nauli za mabasi hayo imepangwa kuwa Tsh. 900
zilizotolewa katika mitandao ya jamii, na kusema huo ni uzushi na
upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili sheria ichukue mkondo.
Alisema
suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya
Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) hivyo uzushi
huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa
kuwapuuzia.
Msemaji
wa Kampuni ya UDA Rapid Transit(UDA-RT),Bw,Subri Maburuki alisema
mabasi yote yameingia yakiwemo ya mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na
huduma ya usafiri kipindi cha mipito itanza baada ya kukamlisha
taratibu za bandari.
“Tuliahidi
kuwa mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni keli
yamemekuja,” na kwa pamoja na yale ya kufundishi yatakuwa jumla mabasi
140", alisema Bw. Maburuki na kufafanua kwamba mabasi hayo yametokea
kiwandani China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT
kama walivyokubaliana.
Kaimu
Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga alisema meli iliyobeba
mabasi hayo ilipitia Kenya na kimsingi ilitokea China ilikuwa imebeba
magari 1700 yakiwemo mabasi ya UDA-RT.
“Hatua
hii ni ya msingi kwa nchi yetu, itasaidia wakazi kusafiri kwa urahisi
na haraka,”alisema Bw. Mhanga. UDA-RT ni kampuni iliyoundwa na wazalendo
kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya DART jijini Dar
es Salaam.
Post a Comment