Tuzo
hizo zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA zinatarajiwa kufanyika Oktoba 8, mwaka huu ukumbi wa
Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo pia TASWA itatoa Tuzo ya Heshima kwa
Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake kwa sekta ya michezo
katika uongozi wake.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja
Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo, alisema
wameamua kusaidiana na TASWA kwa sababu Rais Kikwete ni mdau mkubwa wa
michezo na pia wa masuala ya utalii.
‘’Dk. Kikwete ni mdau mkubwa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwani kwa kipindi chote
ambacho amekuwa Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
hatimaye Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ametembelea hifadhi hii
mara nyingi zaidi kuliko viongozi wengine wote wa Taifa letu
waliomtangulia.
‘’Pia
amekuwa mdau muhimu na wa mstari wa mbele wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro katika kutangaza vyema vivutio vya watalii vya hifadhi ya
Ngorongoro katika mataifa mbalimbali duniani alikokwenda kwa ziara za
kikazi.
‘’Jambo
hili limeleta watalii wengi nchini kutoka mataifa mbalimbali dunini.
Vile vile ziara zake za mapumziko hifadhini wakati wa sikukuu mbalimbali
zimewahamasisha sana Watanzania walio wengi kutembelea hifadhi hii
kutoka kote nchini na hata nchi jirani,’’ alisema Akyoo.
Pia
alisema waandishi wa habari ni wadau wakubwa na muhimu katika harakati
za utalii na ndiyo sababu wameamua kuisaidia TASWA ifanikishe shughuli
yake.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando aliishukuru mamlaka ya
hifadhi hiyo na kusema kuwa msaada huo ni mkubwa na kuomba wadau wengine
waungane nao kufanikisha jambo hilo.
‘’Kama
tulivyosema bajeti yetu ni Sh milioni 130, juzi (Jumatano) tulipata
watu wa GSM Foundation waliotupa Sh. Milioni 50, tunaomba na wengine
tushirikiane nao katika hili,’’ alisema Mhando.
Alisema
TASWA imeamua kuandaa hafla ya wanamichezo kumuaga Rais na pia kumpa
tuzo kwa vile wakati wa uongozi wake amefanya mambo makubwa katika sekta
ya michezo.
Kwa
mujibu wa Mhando, wanamichezo pia watatumia tuzo hizo zilizoandaliwa na
TASWA kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake kikatiba baada ya
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25, mwaka huu.
Post a Comment