Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbrod Slaa, akimjulia hali Askofu wa
kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwenye hospitali ya
kibinafsi ya TMJ
BAADA
ya kutolewa hotuba ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk.Willbrod Slaa wananchi wa mji wa Dodoma
wamepokea hotuba yake kwa mlengo tofauti.
Akitoa
maoni yake Askofu Mkuu wa Kanisa la Endtime Haverst (EHC), Dk. Elias
Mauza amesema alichokifanya Dk. Slaa ni kuacha kuzungumzia hoja na
badala yake amemjadili na kumshambulia mtu mmoja.
“Ni
kweli wanasiasa wengi tuko nao makanisani mwetu na kazi yetu ni
kuhakikisha tunabadilisha mioyo yao lakini ikumbukwe kuwa wananchi
wanahitaji mabadiliko.
“Inapofikia
hatua wananchi wanataka mabadiliko hakuna mtu anayeweza kubadilishwa na
jambo kubwa zaidi kwa wanasiasa wasikubali kutumiwa ili kuwaaminisha
watanzania uongo,” amesema Dk. Mauza.
Kwa
upande wao waendesha bodaboda pamoja na wafanyabiashara ndogo ndogo
wamesema wanachotaka kwa sasa ni madadiliko ya kiuongozi na kiutawala
wala siyo muda wa kuzungumzia mapungufu ya watu wengine.
Mmoja
wa waendesha bodaboda aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Hassani
amesema watanzania wamechoshwa kuishi katika maisha ya ukimbizi.
Naye
Mzee Juma Hassani amesema CCM ni lazima iendelee kushika madaraka na
kitendo cha Dk. Slaa kujiondoa katika siasa ni jambo la ujasiri.
“Tunampongeza
zaidi Dk. Slaa kwa ajili ya kuwaonesha wananchi ukweli na kinachofanywa
na wapinzani amewafungua macho watanzania ambao wanashabikia
wasichokijua,” amesema
Kwa
upande wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu amewataka
watanzania kutokuwa mashabiki wa maandamano ya vyama vya siasa.
Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa alipokuwa akizungumza na Mwanahalisi Online katika mahojiano maaalum.
Shekhe Rajabu amesema wananchi wanatakiwa kuwa makini kwani Tanzania ya leo ni tofauti na ya juzi au ya miaka kadhaa iliyopita.
Amesema
Tanzania ya leo imejaa wasomi tena vijana wadodo wadogo elimu imekuwa
katika kila sekta kiuchumi na kiutandawazi, hivyo wanatakiwa kuwa makini
na viongozi wanaonadi sera zao.
“Tunaelekea
katika uchaguzi hivyo ni vyema tuwe makini na hawa viongozi juu ya sera
zao na tuchague nahodha makini atakayeongoza jahazi letu la jamhuri kwa
mfano au zaidi ya viongozi waluopita,” amesema Shekhe.
Naye
Kiongozi wa kanisa la Gospel Light Ministries International, Mchungaji
Julius Nyange aliwashauri watanzania kutokuwa mashabiki na badala yake
wawe mstali wa mbele katika kupiga kura kuchangua viongozi bora.
Amesema kumekuwa na tabia ya watu kujitokeza kwa wingi katika maandamano mbalimbali ya vyama vya siasa.
Mchungaji
huyo amesema haitakuwa na maana yoyote ile ikiwa watanzania wataishia
kufuata misururu ya vyama vya siasa, huku wakishindwa kupiga kura wakati
wamejiandikisha katika daftali la mpiga kura.
Aidha
amevitaka vyama hivyo vya siasa kuendesha kampeni zake katika kulenga
katika kulinda amani na utulivu bila ya kuleta machafuko.
Chanzo:mwanahalisionline
Post a Comment