Mgombea
wa Ukawa alieteuliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Charles Mabula (kulia)
akipeana mkono na aliekuwa Mgombea wa nafasi hiyo kwa Jimbo la Nzega
mjini, Mezza Leonard (kati) akiekubali kushindwa baada ya kupigwa kura
ya wazi na wananchi wa Nzega Mjini, jana Septemba 6, 2015.Kushoto ni
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ili umasikini unaowakabili
Watanzania uweze kuondoka lazima washirikiane kuiondoa madarakani CCM.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Laini Polisi mjini Nzega, Mkoa wa Tabora ambapo pia alilazimika kuwapigisha kura za mikono wananchi wa Nzega waliohudhuria mkutano huo ili kutatua mvutano wa wagombea wa ubunge katika Jimbo la Nzega Mjini lililokuwa na wagombea wawili wa Ukawa.


Post a Comment