Mhe.
Amos Makalla akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Maji waliompokea
mara baada ya kuwasili Wizarani, pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu, Gideon Manambo.
*******
Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla leo mchana ameaga rasmi
watumishi wa Wizara ya Maji na kwenda kuanza majukumu mapya kama Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe.
Makalla ambaye alifika Wizarani hapo, akitokea Ikulu alikoapishwa rasmi
na Mhe. Rais, Jakaya Mrisho Kikwete, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe.
Makalla ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maji kwa zaidi ya mwaka mmoja,
aliweza kufanya kazi kwa weledi mkubwa licha kuwa mgeni kwenye Sekta
hiyo, ambapo aliweza kuzunguka karibu mikoa yote na kutembelea karibu
Mamlaka zote za Maji nchini katika kukagua utekelezaji na maendeleo ya
miradi ya maji.
Mhe. Amos Makalla akipokea shada la maua kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Beatrice Patrick.
Mhe. Amos Makalla akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maji, wakati akiaga wizarani hapo.
Mhe. Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Maji.
Post a Comment