Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi leo
amefunga fainali za michuano ya kombe la Airtel Rising Stars katika
uwanja Karume jijini Dar es salaam.
Akiongea
kwakati wa ufungaji michuano ya airtel mbele ya halaiki ya vijana
walioshirki michuano hiyo, Malinzi ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel
kwa kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo inawapa nafasi vijana ya
kucheza mpira na kuonekana na baadae kujipatia ajira.
“Lengo
la TFF ni kushirki fainali za Olimpiki za Dunia mwaka 2020 Tokyo –Japan
hivyo wachezaji wenye vipaji kutoka kwenye michuano hii ya Airtel na
vijana wengine wataendelea kutunzwa kwa ajili ya timu ya Taifa ya
baadae” Alisema Malinzi.
Naye
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambao
ndio wadhamini wakuu wa michuano hiyo, amesema airtel wataendelea na
program hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwa wanawake na
wanaume, na kuahidi kuendelea koboresha michuano hiyo kila mwaka.
Michuano
ya Airtel Rising Stars iliyomalizika leo, ilizisihirkisha timu za
wanaume na wanawake kutoka mikoa saba nchini, huku mashindano hayo
yakiwa yanafanyika kwa msimu wa tano sasa tangu kuanzishwa mwaka 2011.
Kwa
upande wa wanaume, timu ya Ilala imeibuka mabingwa baada ya kuifunga
Mbeya kwa mabao 4-0 katika mchezo wa fainali ulochezewa jioni ya leo,
huku timu ya wanawake ya Temeke wakiibuka washindi baaada ya kuibwaga
Kinondoni mwa mikwaju ya penati 5-4.
Post a Comment