JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 22.09.2015.
· MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA BAJAJI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA BASI MALI YA
KAMPUNI YA SAI BABA KUGONGA LORI LILILOKUWA LIMEEGESHWA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ABILAH PHILIMON (17) MKAZI WA
ILEMI, DEREVA WA BAJAJI NA 2. BARAKA SELEMANI (23) MKAZI WA SIMIKE
WALIFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 276 APL
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MAREHEMU KUGONGA GARI T.588 AMR AINA YA
MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL FRANSIS (35).
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO
KIJIJI CHA HATWELO, KATA YA HATWELO, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, WATU SITA KATI YAO WANAUME WATANO NA MWANAMKE MMOJA
WALIJERUHIWA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BAJAJI. MIILI YA
MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA, MAJERUHI WAMELAZWA
HOSPITALINI HAPO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU
MMOJA MKAZI WA TEWELE – NAKONDE –ZAMBIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRAID
AINKALA (67) AFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 630
AFC IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO
KIJIJI CHA NKANGAMO, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA,
BARABARA KUU YA TUNDUMA/SUMBAWANGA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, WATU WAWILI WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. MAGRETH MTAMBO
(52) NA 2. ANASTAZIA NYAMUNGALA (55) WOTE WAKAZI WA KAKOZI –NAKONDE –
ZAMBIA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA MAJERUHI WAMELAZWA KITUONI HAPO.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU
MMOJA AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA LAKE, TINGO WA BASI MALI YA KAMPUNI YA
SAI BABA AFARIKI DUNIA BAADA YA BASI HILO LENYE NAMBA ZA USAJILI T.668
BLD AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA
SUMBAWANGA KUGONGA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.771 ATV/T.771 AUU
SCANIA LORI ILIYOKUWA IMEEGESHWA BAADA YA KUHARIBIKA ENEO LA MLIMA
NYOKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO
ENEO LA MLIMA NYOKA, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, ABIRIA WAWILI AMBAO PIA MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA
WALIJERUHIWA NA WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI WA BASI HILO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA
ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA BASI LA SAIBABA AZITOE
ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO
AJISALIMISHE MWENYEWE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment