Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Joseph Musukuma Amshambulia LOWASSA........Asema Alijisaidia Hadharani Pale Chato. Tazama Video hii




MWENYEKITI wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemvaa mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa na wengine waliohamia Ukawa akisema wanashukuru chama kimetua mzigo.
 
Msukuma, ambaye anaaminika kuwa swahiba wa Lowassa wakati wa mchakato wa kura ya maoni kwenye CCM, aliuambia mkutano jana kwamba hakuna anayefahamu siri za Lowassa.

 
“Nataka nimwambie ndugu yangu, rafiki yangu Lowassa, huu ni muziki mkubwa,” alisema Msukuma kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa CCM, Dk John Magufuli uliofanyika jana mjini Chato, mkoani Geita.

 
Msukuma ambaye aliponda waliohama CCM baada ya kura za maoni kwa kutaja majina ya baadhi, akiwalinganisha na bendera inayofuata upepo na kusisitiza kuwa wenye akili hawahami.

 
“Tumeshukuru sana CCM tumetua mizigo…”, alisema Msukuma ambaye ni mgombea ubunge, Jimbo la Geita Vijijini akiwataja Lawrence Masha, Msindai, Mngeja akisema wamehamia Ukawa si kwa mapenzi mema isipokuwa, ni kutokana na kukosa ushindi kwenye kura za maoni.

 
“Tuna hasara gani Masha akihama CCM?” alihoji umati ambao uliitikia kwa kusema hakuna hasara. 

 
Msukuma ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa CCM waliohudhuria mkutano wa Lowassa uliofanyika Arusha wakati wa mchakato wa kura za maoni, akisifia mkutano wa jana wa Magufuli, alisema, “Toka niwe mwenyekiti sijawahi kuona watu wengi kama hawa. Hata nilipoteremka Arusha na chopa, haikuwa hivi.” 


Alieleza kushangazwa na baadhi ya picha zilizooneshwa kuwa ni za mkutano wa Lowassa mjini Chato na kusema mandhari iliyooneshwa, haikuwa ya uwanja huo wa stendi.

 
“Stendi ya Chato haina miembe wala lami,” alisema. Akiendelea kuponda waliohama, alisema, kama Dk Magufuli angekuwa anatoa rushwa, wasingehama. 

 
“Hakuna hasara na wote waligombea wakashindwa,” alisema na kueleza kumfahamu Mngeja kwa kuwa walikuwa wakikaa kwenye helikopta moja.

 
“Tunaomba wachukue na wengine wenye tabia kama hizo. Wenye akili timamu tutabaki CCM...Mgombea wetu (Magufuli) anatosha. Na hapa ndiyo kwao…nimetembea na Lowassa gari moja, ndege moja, tunachagua rais na sio bora rais…,” alisema.

 
Alisisitiza, “Katika Kanda ya Ziwa, hakuna aliye na siri za Lowassa kama mimi…naomba waniweke kwenye mdahalo nitagharimia, niwapige kavu kavu. Watu wanaokwenda kule (Ukawa) zinatangulizwa hela. Nani anachukia hela?.”

 
Aliendelea kusema, “najua mengi ya kambi ile nilikwenda kufanya kazi. Hata wale wachungaji waliokwenda Dodoma, ni wachungaji feki walionunuliwa.”


Baada  ya  hapo, Msukuma  aliwauliza  maelfu  ya  wananchi  kuwa...." Mgombea  wa  UKAWA  alifanya  nini  pale  stendi?"......Wananchi  Wakamjibu...."Alijinyeaaaaa"


Msukuma akasema, "Sijasikia", Wananchi  wakajibu...."Alijinyeaaaa".


Akasema  tena, " Alijinyee......!!!". Wananchi  Wakamalizia..."aaaaaa"


Zaidi, Tazama  video  hapo  chini  kumsikiliza

M
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top