Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Lowassa atua Mtwara kwa kishindo


Lowassa atua Mtwara kwa kishindo
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) pamoja na UKAWA, leo ameanza kampeni kanda ya kusini akianzia Mtwara.

Mkoani Mtwara Lowassa amepokewa na umati wa Wananchi, mji wa Mtwara na viunga vyake vyote ulizizima, shughuli nyingi zilisitishwa wengi wakijongea kumsikiliza Waziri Mkuu huyo mstaafu.
Mh.Edward Lowassa amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa serikali yake ya awamu ya tano itajikita katika kuimarisha uchumi ikiwa ni pamoja na kuwafanya wakazi wa mji wa Mtwara kunufaika kikamilifu na rasilimali za gesi na mafuta huku akiwahakikishia pia upatikanaji wa soko la uhakika la mazao ya Korosho.
Naye Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu, amewataka wakazi wa Mtwara kuhakikisha wanamchagua kwa kura nyingi Edward Lowassa kwani kushindwa kufanya hivyo ni kuifanya Mtwara na mikoa ya kusini kwa ujumla kuzidi kuwa nyuma kimaendeleo.
Kutokana idadi kubwa ya maelfu wanaozidi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Edward Lowasa, viongozi wa ngazi ya juu wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, wanaamini ni dhahili mabadiliko ya Oct 25 hayakwepeki.
Akiwa mkoani Mtwara na timu yake ya kampeni Edward Lowassa alifanikiwa kuhutubia mikutano mikubwa ya hadhara katika majimbo ya Tandahimba, Newala kabla ya kuhitimisha katika uwanja wa mashujaa ambapo hata hivyo uwanja huo ulijikuta ukishindwa kuhimili kishindo cha mgombea huyo wa nafasi ya urais.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top