Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Emmanual Mbasha (32), leo ameangua kilio baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Ilala huku mke wake, Flora amesema yuko tayari warudiane endapo ataomba radhi.
Mbasha alimwaga chozi muda mfupi baada ya kutoka katika chumba cha Mahakama alipopandishwa kizimbani kusomewa hukumu.
Mshtakiwa
huyo ameachiwa huru dhidi ya kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili baada
ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kosa.
Mwimbaji
huo ambaye kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo alionekana hana furaha,
alifikia uamuzi huo wa kulia mara tu baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo,
ambapo alipotoka nje ya chumba cha mahakama alipiga magoti chini huku
akiinua mikono juu na kulia kwa sauti huku akisema ‘mungu ni mwema’.
Mbasha
anakabiliwa na mashtaka mawili ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa
miaka 17 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria
Kesi
hiyo namba 186 ya mwaka 2014, imeendeshwa kwa mwaka mmoja na miezi
miwili na kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Juni 17 mwaka
2014.
Akisoma
hukumu hiyo leo, hakimu Mkazi Flora Mujaya alisema mahakama imemuachia
huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kosa lililokuwa
likimkabili.
“Mahakama yangu imemuachia huru Mbasha baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kosa ”alisema Hakimu Mujaya.
Hakimu
Mujaya alisema mahakama hiyo imetoa uamuzi huo baada ya kupitia
ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka vikiwemo vielelezo
vilivyotolewa mahakamani hapo kama ushahidi.
Hukumu
hiyo, ilipaswa kutolewa wiki iliyopita , lakini iliahirishwa hadi leo
kwa sababu hakimu huyo ambaye ametoa hukumu hiyo leo alikuwa likizo .
Mke
wa Mbasha, Flora alisema yeye na familia yake wanaheshimu maamuzi
yaliyotolewa na Mahakama dhidi ya Mbasha na kwamba anaiomba familia yake
ikubaliane na maamuzi hayo na suala la kukata rufaa lisiwepo.
“Mimi
na familia yangu tunaheshimu uamuzi wa mahakama na ninaiomba familia
yangu ikubaliane na uamuzi huu uliotolewa na mahakama na suala la kukata
rufaa lisiwepo kwani uamuzi wa mwisho upo katika familia” alisema Frola
alipotafutwa kwa simu.
Post a Comment