JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA
YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA (TAWA)
Wizara ya Maliasili na
Utalii inapenda kuujulisha umma kuwa, Bodi mpya ya Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife
Authority -TAWA), imeteuliwa rasmi
kuanzia tarehe 09 mwezi Septemba, 2015.
Katika uteuzi huo, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Rajabu SEMFUKO kuwa
Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ambao wameteuliwa na Waziri wa
Maliasili na Utalii ni Dkt. Simon Mduma – Mkurugenzi Mkuu - TAWIRI,
Dkt.
Fred Manongi – Mhifadhi Mkuu - NCAA,
Suzane
Charles Ndomba – Mwanasheria – ATE, Bw.
Gerald Bigurube – Meneja wa Program Frankfurt Zoological Society – SERENGETI, Dkt.
David Manyanza (Mstaafu) Mtaalam wa
Maswala ya Wanyamapori , Bw. Benson A. Shallanda – Kamishna wa Sera – HAZINA, Jenerali Samweli Ndomba – Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi, Winfrida Nshangeki – Mkurugenzi wa Uratibu wa Sera – TAMISEMI,
Abdulrahman Kaniki – Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania , Allan J. Kijazi –
Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mr. Herman W. Keraryo
–Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Abdul Rajab Mhinte – Mkuu wa Idara
ya Usalama na Atakayeteuliwa
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka.
Bodi hii, itaongoza Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe ya uteuzi.
Imetolewa
na
Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikali
Wizara ya Maliasili na Utalii
21/09/2015
Post a Comment