………………………………….
Wanafunzi wanaosoma masomo ya
Sayansi kote nchini wameshauriwa kuongeza bidii katika kujifunza masomo
hayo ili kuendana na juhudi zinazofanywa na Serikali za kuwawezesha
wanafunzi hao kujifunza masomo ya Sayansi kwa vitendo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samweli Manyele kwenye sherehe
ya kuwapongeza wanafunzi 24 wa kidato cha nne na sita waliofanya vizuri
katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa mwaka 2013 na 2014.
“Kama wachunguzi wa Serikali
ambao hutumia taaluma zitokanazo na masomo ya Kemia na Biolojia tumeona
ni Vizuri kutoa hamasa kwa vijana na Taifa hili kupenda masomo ya
Sanyansi” Amesema Prof. Manyele.Amesema Zoezi la kuwapongeza na
kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya Kemia na
Biolojia limeanzishwa kutoakana na Wakala ya Mkemia Mkuu wa Serikali
kupewa jukumu la kusimamia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali
za Viwandani na Majumbani.
Aidha, amesema Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania kitagharamia masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
kwa walimu na wanafunzi wanne ili waweze kuimarisha vipaji vyao vya
masomo na matumizi ya kompyuta .
Amefafanua kuwa Katika sherehe
hizo jumla ya wanafunzi 24 na walimu 4 kutoka shule mbalimbali za
Sekondari hapa nchini wamezawadiwa vitu mbalimbali zikiwemo Fedha, Vyeti
na Santuri kwa ajili ya kujifunza zaidi masomo ya Sayansi kwa upande wa
wanafunzi na walimu kujifunza mbinu zaidi za kufundisha masomo hayo.Kwa upande wa Wanafunzi
waliozawadiwa amesema wanatoka shule za Sekondari za Feza, Marian,
Iliboru, St. Francis na Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamanoro iliyoko
jijini Mwanza.
Sherehe za kuwazawadia na kuwapa
tuzo mbalimbali wanafunzi wa masomo ya Sayansi zilianzishwa mwaka 2007
chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali, huambatana na utoaji wa zawadi na
tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia
na Bioloji.
Post a Comment