Askari mgambo 114 wilayani Handeni wametishia kugoma kwenda kusimamia vituo vya kupigia kura kutokana na kutolipwa fedha zao kama walivyokubaliana na mkurugenzi.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti leo mgambo hao wamesema kuwa katika makubaliano yao
walisaini hela yote lakini kwenye malipo walipewa nusu ya hiyo hela
ambapo ni kinyume na maelewano ya awali.
Seiph
Mhando askari kata ya Chanika wilayani Handeni ambae ndio kiongozi wa
mgambo hao amekiri kutokea kwa kutoelewana huko kuwa mgambo hao
walikataa kupewa pesa nusu na ikiwa hivyo hawatakwenda kulinda vituo.
Amesema mgambo walitaka fedha kama walivyosaini na ikiwa haitakuwa hivyo maamuzi yao yatakuwa ni yale Yale.
Akifafanua
suala hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Handeni mjini
Keneth Haule amesema ni kweli kulitokea tatizo hilo ambapo mgambo hao
114 wametaka kulipwa fedha zote ila taratibu zinabana kufanya hivyo.
Ameeleza
kuwa ni kweli kuna makosa yalifanyika kwa kuwaeleza kiasi chote
watakacholipwa lakini wakawapa nusu lakini walikata na kutaka kulipwa
fedha yote kama walivyokubaliana kwenye mkataba wa awali.
Haule
amesema sababu ya kutotoa fedha zote ni ili kuweza kujikinga na dharura
yoyote itakayoweza kutokea kwa mmoja wa askari hao ila kwasababu
wametaka kulipwa fedha zote wameshawalipa.
Ameongeza kuwa kwa kuwa kila mgambo atakabidhiwa vifaa basi ndio itakuwa dhamana kwa kila askari.
Kuhusu
maandalizi ya uchaguzi kesho ameeleza kuwa yapo vizuri hakuna tatizo
lolote lililoripotiwa kwenye eneo lake na mambo yote kesho yatakwenda
vizuri.
Post a Comment