Mwenyekiti
wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray akizungumza na Waandishi
wa Habari kuhusiana na kutafakari mwenendo wa Kampeni unavyoendelea
na Changamoto na Utatuzi wake katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani
Zanzibar,kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Fedha ya Baraza la vyama vya
Siasa Constantine Akitanda na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
na Siasa ya Baraa la vyama vya Siasa Lifa Chopaka.
-Baadhi
ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano na Mwenyekiti wa
Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray kuhusiana na masuala
mbalimbali ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar.Picha
na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Baraza
la Vyama vya Siasa nchini limevishauri vyama vya siasa kuzungumza na
kuwasihi wafuasi wao kutii sheria bila shuruti ili kuendeleza amani
iliyopo nchini.
Aidha
Baraza hilo limeviomba Vyama kuwaeleza wafuasi na wapenzi wao kurudi
majumbani na kuendelea na shughuli zao mara baada ya kupiga kura siku ya
uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa hatua za uandikishwaji.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray
wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Kikako
maalumu cha Baraza hilo kilichofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini
Zanzibar.
Kikao
hicho kilitafakari mwenendo wa Kampeni za Wagombea katika ngazi
mbalimbali na kujadili changamoto mbalimbali na utatuzi wake ili
kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki na kufanyika katika mazingira
ya Amani na Utulivu.
Mziray
amefahamisha kuwa wamekubaliana katika kikao hicho kuwa Wapiga kura
wana haki kama watapenda mara baada ya kura kuhesabiwa na matokeo
kubandikwa kwenda Vituoni hapo kwa ajili ya kuangalia Matokeo kwa wakati
wanaopenda.
Aidha
amesema Vyama pia vimesisitizwa kuweka Mawakala wanaowaamini katika
Vituo vya kupigia kura ambao watajumuisha kura za Wagombea katika nafasi
za Madiwani, Wabunge na Rais katika maeneo husika.
Mziray
ameongeza kuwa Baraza la Vyama vya siasa pia limeshauri Vyama hivyo
kuzingatia na kuweka amani ya nchi mbele kwa maslahi ya Taifa.
“Katiba
ya Nchi iko wazi kuwa atakayeshinda kwa kura nyingi ndiye
atakayetangazwa na kupewa cheti na Tume ya uchaguzi” alisema Mziray
Ametoa
rai kwa Katibu Mkuu kiongozi kuratibu shughuli za kuapishwa Rais ambaye
kwa mujibu wa Sheria huapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya
kutangazwa ndani ya kipindi kisichozidi siku saba.
Mzirai
pia ameelezea kufarijika kwao na Tume ya Uchaguzi kwa kuvihakikishia
Vyama vya siasa kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na kwamba Mgombea
atakayeshinda kwa kura nyingi zaidi na halali ndiye atakayetangazwa kuwa
Mshindi.
Mzirai
amevimetaka Vyama vya siasa kuwaasa Wagombea wao kukubali Matokeo kama
yatakavyotangazwa na Tume ya uchaguzi ya kushinda au kushindwa.
Kwa
upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Damian
Lubuva na Mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Khamis Khamis
wakati wakiwasilisha mada juu ya usimamizi na utekelezaji wa maadili
Uchaguzi nchini wamevitaka Vyama vya sias kuendelea kuzingatia maadili
ya uchaguzi kwa kuwa shauku ya kila Mtanzania ni kuona uchaguzi unaisha
kwa amani.
Kikao
hicho maalum cha cha siku mbili cha Baraza la Vyama vya Siasa
kilijumuisha Wajumbe kutoka Baraza hilo, Wageni kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi NEC, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC na Jeshi la Polisi na
kuandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini.
Baraza
la Vyama vya Siasa limeundwa chini ya kifungu 21B cha Sheria ya Vyama
vya siasa Namba 5 ya mwaka 1992 kama ilivyorekebishwa na Sheria namba 7
ya mwaka 2009.
Post a Comment