Msanii Bond Suleiman ‘Bond’ na Wasstara.
Brighton Masalu
KUTOKANA na ugumu wa masharti aliyopewa
na mwigizaji Wastara Juma juu ya kumuoa, msanii Bond Suleiman ‘Bond’
ameomba msaada kwa watu wa karibu hususan upande wa Wastara kumsaidia
kumuweka sawa ili atimize lengo lake la kumuoa.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi
karibuni, Bond alisema Wastara ni mwanamke mwenye kila sifa ya kuwa mke,
hivyo endapo atamkosa litakuwa ni pigo kubwa maishani mwake.
“Jamani, amenipa masharti magumu sana,
ni mwanamke thabiti ambaye nisingependa kumkosa, najaribu kuwatumia watu
wetu wa karibu kumuweka sawa, maana ana kila sifa za kuitwa mke,
nimekaa naye muda mrefu kama meneja wake, nimegundua mambo mengi sana,
nahitaji msaada jamani,” alisema Bond.
Post a Comment