Mgombea
urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad,
ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema kuwa baada ya chama
chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni, yeye amepata kura
200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake,
Dk. Ali Mohammed Shein.
Aidha,
akiongea na wanahabari, Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye
fomu zinazotoka vituoni.
Chanzo: DW
Post a Comment