Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva imemtangaza Rasmi mgombea Urais wa CCM, Dr John Pombe Magufuli kuwa mshindi halali wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.
Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr magufuli amepata ushindi wa kura Milioni 8 ( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.45%
huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu , Edward
Lowassa (Chadema ) ambaye amepata jumla ya kura Milioni 6 (
6,077,848 ) sawa na asilimia 39.97%
Aliyeshika nafasi ya tatu ni mama Anna wa ACT aliyepata 0.65%, huku Chief Yemba wa ADC akipata 0.43%, wa tano ni Hashim Rungwe wa CHAUMMA 0.32%, huku NRA, TLP na UPDP wakipata wote asilimia 0.05.
Aliyeshika nafasi ya tatu ni mama Anna wa ACT aliyepata 0.65%, huku Chief Yemba wa ADC akipata 0.43%, wa tano ni Hashim Rungwe wa CHAUMMA 0.32%, huku NRA, TLP na UPDP wakipata wote asilimia 0.05.
Dr
Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu watakabidhiwa rasmi
vyetu vya ushindi kesho saa nne asubuhi katika ukumbi wa
hoteli ya Diamond Jubilee
Post a Comment