THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Ndugu Natu Rashid Msuya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF).
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi, Oktoba 29, 2015 Ikulu, Dar
es Salaam na Katibu Mkuu - Ikulu, Ndugu Peter Ilomo uteuzi huo ulianza
Jumapili ya Oktoba 25 mwaka huu, 2015 na ni wa miaka mitatu.
Bibi Natu Msuya ni Mshauri wa Wanafunzi, Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE cha Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Oktoba, 2015.
on Friday, October 30, 2015
Post a Comment