TIMU ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inatarajiwa kusafiri na ndege ya binafsi ya kukodi ya shirika la Fastjet kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Novemba 17 mjini Algiers.
Meneja
Mkuu wa Shirika la Ndege la Fasjet kwa ukanda wa Afrika Mashariki,
Jimmy Kibati amesema kampuni yao imefikia makubaliano na TFF ya kuwa
msafirishaji rasmi wa timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo huo wa kuwania
kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi 2018 dhidi ya Algeria.
Jimmy
amesema katika safari hiyo, Fastjet itatoa ndege yenye uwezo wa kubeba
abiria 156 walioketi, sambamba na wafanyakazi wa ndenge, ambapo wao
wametoa punguzo la asilimia 35 katika gharama nzima ya safari ya
kuelekea Algeria.
Aidha
Jimmy ameongeza kuwa safari hiyo itakua ni ya masaa 7 ambapo ndege
ikitoka Dar es salaam itatua Djamena – Chad kuongeza mafuta kabla ya
kuendelea tena na safari mpaka nchini Algeria.
Naye
katibu wa kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda aliwashukuru Fastjet kwa
kukubali kuwa wasafirishaji rasmi wa TaifA Stars kwa mechi dhidi ya
Algeria, huku akisema gharama za safari za mtu mmoja kusafiri ni dolla
800 kwenda na kurudi.
Teddy
amewaomba watanzania, wapenzi, washabiki wa mpira wa miguu wanaotaka
kusafiri kufika ofisi za TFF zilizopo Karume kwa ajili ya kujiandiksha
na kuelekea taratibu nzima za safari.
Post a Comment