Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limetuma salamu za pongezi kwa viongozi
wa mpira wa miguu nchini waliochaguliwa kuwa wabunge na madiwani katika
uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Viongozi
waliochaguliwa katika nafasi ya Ubunge ni John Kadutu – mbunge wa
Ulyankulu – Tabora, (mjumbe wa mkutano mkuu kutoka Mwanza) na Alex
Gashaza – mbunge wa Ngara (Makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa
Kagera)
Aidha
waliochaguliwa Udiwani katika maeneo yao ni Khalid Abdallah (Mjumbe wa
kamati ya Utendaji – TFF), Yusuph Kitumbo- (Mwenyekiti wa Chama cha
Mpira wa Miguu mkoa wa Tabora), Omari Gindi- (Mwnyekiti wa Chama cha
mpira wa Miguu mkoa wa Kigoma), Bathromeo Kimaro - (Mwenyekiti wa Chama
cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida) na Omar Kinyeto (Mjumbe wa mkutano
mkuu mkoa wa Singida), Golden Sanga (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa
Miguu mkoa wa Ruvuma), Pachal Kihanga (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa
mkoa Morogoro), Yusuf Manji (Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC) ambao wote
ni wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF.
TFF
inawaomba kutumikia halmashauri zao kwa mafanikio na kutilia mkazo
kuhifadhi maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo mbalimbali hususani mpira
wa miguu mashuleni.

Post a Comment