CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium
Tower, wakili wa Chadema, John Mallya alisema Rais Kikwete ameshitakiwa
Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa
sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi
mkuu.
Mallya
alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia
nakala za tuhuma dhidi ya Rais Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika
(AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue
Uholanzi.
Kwa
mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Rais
Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah
Safari.
Mashataka
haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete ailaumu
Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii
kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa
kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.
Kauli
hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua
mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi
Kusini mwa Afrika-SADC,
Hiyo ilikuwa ni siku moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.
Mwendesha
Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari
vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa
umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama
ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba
itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.
Kauli
hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.
Lowassa
alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa
ya Arusha na Mwanza kwa kulitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo
wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya
wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.
Post a Comment