Mgombea
urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ametuma salamu
za rambirambi kwa Jeshi la Polisi, kufuatia kifo cha askari wa Kikosi
cha Usalama Barabarani, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, aliyepata ajali
wakati akiongoza msafara wake.
Taarifa
iliyotolewa jana na CCM kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa, Dk.
Magufuli alipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha askari
huyo, F.4946 PC. Essaya ambaye alipata ajali juzi wakati akiongoza
msafara wa mgombea huyo wa urais na kupoteza maisha eneo la Ubungo
Mataa, jijini Dar es Salaam.
Dk.
Magufuli katika salamu zake za rambirambi alizomtumia Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, alisema:
“Kwa hakika, nimeshtushwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za kifo cha F.
4946 PC. Essaya ambacho kimetokea baada ya kupata ajali ya kugongana na
pikipiki (Bodaboda) iliyoingilia msafara wangu uliokuwa ukitokea Lugalo
kwenda Vingunguti, jijini Dar Es Salaam."
Aidha, alimuomba Inspekta Mangu, kumfikishia salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na rafiki wa marehemu.
"Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.
Pia
namuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema
peponi, kazi ya Mungu haina makosa,” ilisema taarifa hiyo ikimnukuu,
Dk. Magufuli.
Post a Comment