Dar es
Salaam. Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka atapanda ulingoni mjini
Manchester Uingereza Novemba 7 kupambana katika pambano lisilokuwa la ubingwa.
Akizungumza
kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security
Limited, Juma Ndambile amesema kuwa Cheka anatarajia kuondoka wiki ijayo kwa
ajili ya pambano hilo.
Ndambile
ambaye ni meneja wa Cheka, alisema kuwa tayari msaidizi wake, Rashid Nassoro
yupo nchini Uingereza akiwa na mabondia wengine wawili huku akikamilisha
maandalizi ya mwisho ya pambano hilo.Kwa mujibu
wa Ndambile, Cheka anaweza kupambana na mpinzani wake wa awali, Martin Murray
au bondia mwingine kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.
“Maandalizi yanaendelea vizuri na msaidizi
wangu, Rashid Nassoro, kwa sasa yupo Uingereza akikamilisha masuala ya pambano
hilo, kuna vitu fulani fulani vilikuwa havijakamilika, ila pambano ni Novemba 7
na leo jioni nitajua lini tutaondoka Tanzania,” alisema Ndambile ambaye kwa
sasa yupo Kenya kikazi.Alisema kuwa
Cheka kwa sasa yupo mkoani Morogoro akiendelea kujiandaa na pambano hilo na
kama unavyojua, akishinda, atapata ofa kubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
Alisema kuwa
Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya
dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata
la ubingwa
“Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata
akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia
nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato,
nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.
Alisema kuwa
Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea
kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.
Wakati huo
huo; Bondia Benki Mwakalebela ambaye alitakiwa kupanda jukwaani jana usiku,
hakuweza kufanya hivyo baada ya pambano lake kuhairishwa dakika za mwisho.
Ndambile
alisema kuwa Mwakalebela alitakiwa kupambana na bondia Craig Kennedy na pambano
hilo limefutwa kutokana na sababu za kiufundi.
Post a Comment