Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hakuna malalamiko yoyote yaliyowasilishwa katika siku ya upigaji kura.
Maalim
Seif ambaye ni Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF ametoa kauli
hiyo baada ya kuwepo taarifa kuwa mawakala wa CCM wameitwa pamoja na
maofisa wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) katika kiwanda cha Makonyo
Wilaya ya Chake Chake, kwa ajili ya kujazishwa fomu za malalamiko ili
ziweze kutumika kudai kuwa yalikuwepo malalamiko katika zoezi hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho zilizoko Mtendeni
Mjini Zanzibar, Maalim Seif amesema njama hizo za CCM wameshazigundua na
kawatozikubali.
Amesema
njia pekee ya kuondosha utatanishi wa uchaguzi huo ni kukamilisha
uhakiki wa majumuisho na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Amesema
kwa upande wake pamoja na Chama chake, wataendeleza jitihada za
kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa,
ili kukamilisha uhakiki wa majumuisho ya kura kwa majimbo 14 yaliyobaki
na hatimaye kutangazwa mshindi wa Urais si zaidi ya tarehe 02/11/2015.
Hata
hivyo amesema iwapo hakutokuwa na hatua zozote zilizochukuliwa
kukamilisha uchaguzi huo na kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi
hadi ifikapo tarehe 01/11/2015, viongozi wa CUF wataondoa mkono wao na
kuwaachia wananchi waweze kutafuta haki yao kwa njia za amani.
Katika
hatua nyengine Maalim Seif ameelezea kusikitishwa na vitendo
vinavyofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuwatesa na kuwapiga
raia wasiokuwa na hatia katika makaazi yao.
Amesema
matukio hayo yamekuwa yakiripotiwa zaidi katika Wilaya za Magharibi “A
na B”, na katika tukio la hivi karibuni amesema nyumba za raia wasiokuwa
na hatia zimechomwa moto katika kisiwa cha Tumbatu na kuwafanya
wananchi kuanza kupoteza uvumilivu.
Post a Comment