Madereva
wa magari ya kubeba mizigo jana asubuhi wameweka kizuizi katika eneo la
Misusugu, barabara kuu ya Morogoro wakilaani kuuawa kwa dereva mwenzao
aliyefahamika kwa jina la David Mwakalinga juzi eneo la Mbagala jijini
Dar es Salaam
Inadaiwa
dereva huyo amepoteza maisha kwa kupigwa risasi na mwajiri wake. Kwa
mujibu wa madereva hao marehemu David Mwakalinga alikuwa mfanyakazi wa
kampuni iliyotajwa kuwa Triple A.
Hatua
ya kuweka kuzuzizi hicho ilisababisha msongamano mkubwa wa magari
katika eneo la Misugusugu hadi kwa Mathias Kibaha mkoa wa Pwani hali
iliyodumu kwa takriban saa saba na kusababisha usumbufu mkubwa kwa
madereva wengine pamoja na wasafiri.
Wakiongea
na Channel Ten katika eneo la tukio, baadhi ya madereva wamedai kuwa
kwa muda mrefu wamekuwa wakinyanyaswa na baadhi ya waajiri ikiwemo
kunyimwa haki za msingi na kwamba baada ya kupokea taarifa ya mazingira
ya kifo cha mwenzao wameamua kuonyesha hisia zao kwa kufunga barabara
mpaka alipofika mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Ernest Ndikilo na kuanza
majadiliano nao ambayo hatimae yalizaa matunda
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa TADWU mwili wa marehemu ulihifadiwa katika
hospitali ya taifa Muhimbili huku mtuhumiwa wa mauaji hayo akidaiwa
kuwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha Polisi Chang'ombe. Mkuu wa Mkoa
wa Pwani hakuwa tayari kusema lolote kwa kudai tukio la mauji limetokea
nje ya eneo la mamlaka yake na kwamba yupo eneo la mgomo kusaidia
kuondoa kizuizi barabarani. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani Jaffar
Ibrahim amethibitisha kutokea kwa mgomo huo wa madereva kufuatia kifo
cha dereva mwenzao
Post a Comment