Mgombea
Mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia
Suluhu Hassan (kushoto), akizungumza katika mkutano uliowakutanisha
wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wajasiriamali pamoja na
wanachama kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata),
baada ya kupokea changamoto zao Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam
leo.
Mmoja wa viongozi kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), Nasria Nasri (kushoto), akimueleza Mama Samia changamoto walizonazo.
Mhasibu
wa Kitengo cha Fedha, Magogoni, Charles Temba akizungumza katika
mkutano huo kuhusu changamoto mbalimbali ambapo alimuomba mama Samia,
watu wenye ulemavu watengewe luzuku.
Mwakilishi wa Walemavu, Kuruthum Dindili akimueleza Mama Samia changamoto walizonazo.
Musa Hassan akimueleza Mama Samia changamoto walizonazo.
Mwakilishi
wa Wajasiriamali kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Siriel
Mchemba akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto walizonazo.
Mgombea
Mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia
Suluhu Hassan (kushoto), akipunga mkono kuwasalimia wanachama wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT), Wajasiriamali pamoja na wanachama kutoka
Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), wakati akiingia
ukumbini kwenye mkutano wa kupokea changamoto zao Ukumbi wa Diamond
Jubilee Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia
Simba
Wanachama kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), wakiwa kwenye mkutano huo.
Wakina mama wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanamuziki,
Khadija Shabani 'Keisha' akiimba wimbo maalumu wa kampeni katika
mkutano wa Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama cha
Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan uliowakutanisha wanachama wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT), Wajasiriamali pamoja na wanachama kutoka
Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), baada ya kupokea
changamoto zao Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam
Mmoja wa wanashirikisho la walemavu akishangilia jambo.
Na Dotto Mwaibale
MGOMBEA
Mwenza wa Chama cha Mapinduzi Samia Suluhu Hassan amewaahidi watu
wenye ulemavu kuwa atashirikaina nao katika changamoto zao
zinazowakumba.
Akizungumza
Dar es Salaam leo katika mkutano uliwakutanisha Umoja wa Wanawake
Tanzania wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Shirikisho la walemavu
(Shivyata), Samia alisema atawasaidia walemavu kwa uwezo wao na si kwa
ulemavu wao.
"Katika
serikali yangu nitahakikisha kuwa tunawasaidia walemavu kwa uwezo wao
na sio kwa ulemabvu wao kwani walemavu wanao uwezo wa kufanya chochote
kama watu wengine,"alisema.
Alisema
katika kuwasaidia walemavu hao ni lazima kuwaandalia mazingira ya
miundombinu iliyo bora mitaji ya kuwakwamua kiuchumi na kuondokana na
umaskini.
Pia
alisema katika serikali yake kutatengwa maeneo maalum kwa ajili
wafanyabiashara na masoko matatu kwa jiji la Dar es Salaam yaani katika
wilaya ya Ilala,Temeke na Kinondoni.
"Tutaiyomba
Halmashauri za manispaa kutengwa maeneo maalum maalum kwa ajili ya
wafanya biashara ndogondogo pamoja na kuiwepo na mamlaka maalum ambayo
itashghulika na sekta hiyo isiyo rasmi kwani kwa sasa halmashauri
zinawatoza kodi kwa kuamua wenyewe,"alisema.
Alima
katika harakati hizo kutaingwa taasisi ambayo itatengewa sh.bilioni 10
ambayo itawafanya nma kuunganishwa katika mfuko wa hifadi za jamii na
itasimamiwa kwa uimara wa hali ya juu.
Akiwazungumzia
wananchi wa vijijini Suluhu alisema katika srikali yake kutatengwa
milioki 50 kwa kila kijiji lengo likiwa kuwapatia maendeleo na
kukopeshwa kwa ajili maendeleo.
Kwa
upande mwingine Suluhu aliwazungumzia wazee na kusema hasa wale wazee
ambao hawajaajiriwa na serikali kwa kuandaa taasisi ambayo itakuwa
inawashughulikia wazee.
"Tutapitisha
sensa ya wazee na kuweza kufahamu wazee wako wangapi ili kuweza
kuwasaidia na kuwapa mafao ambayo itawasiadia kwa kiasi
kikubwa,"alisema.
"Awamu
ya tano tumejipanga kwani hapa ni kazi tu,tukopesheni kura na sisi
tutawalipa masendeleo pamoja na kututafutia kura katika kila
eneo,"alisema.
Kabla
Mgombea huyo hajaanza kuongea mmoja wa majsiramali alisema Siriel
Mchembe alimweleza mgombea huyo kuwa wanahitaji maeneo ambayo itakuwa
hawafukuzwi na migambo.
Aidha
mmoja wa walemavu kutoka katika kijiji cha feri Charles Temba alisema
wanahitaji sehemu ambayo ya kupaki bajaji zao kutokana na magari ya
mwendo kasi kuanza.
Kwa
upande mwingine mlemavu wa ngozi Mussa Hassan alimwambia mgombea huyo
kuwa iwe mstari wa mbele kuwatetea walemavu wa ngozi hasa katika masuala
kuuliwa kisa tu ni walemavu.
Post a Comment