Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini . Jaji Francis S. K Mutungi akizungumza na Waangalizi wa uchaguzi Mkuu kutoka
Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo jana Oktoba 21,2015.
Baadhi ya Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
kushoto ni Msajili Msaidizi Usajili wa Vyama vya Siasa Bw. Sisty Nyahoza akielezea utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa , kulia ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji francis Mutungi.
Picha
ya pamoja ya Jaji Francis S.K Mutungi , Waangalizi wa Uchaguzi kutoka
Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na
baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
TUME
ya Uchaguzi ya Taifa nchini NEC imewataka waangalilizi wa uchaguzi
kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ya waangalizi wa uchaguzi katika
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu.
Hayo
yaliyasemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji mstaafu
Damian Lubuva alipokuwa akizungumza na waangalizi wa uchaguzi mkuu
kutoka nchi za Jumuiya ya Madola uliyofanyika jana jijini Dar es
Salaam.
“Tunataka
amani na utulivu wa nchi uendelee kuwepo hata baada ya uchaguzi hivyo
fanyeni kazi yenu ya uangalizi kwa kuzingatia sheria na msikiuke
misingi ya sheria hiyo”,alisema Jaji Lubuva.
Akizungumza
kuhusu maswali waliyomuhoji waangalizi hao Jaji Lubuva
alisema waangaliza hao walizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo
maandalizi ya uchaguzi kwa upande wa Tume ikiwa ni pamoja na usambazaji
wa vifaa, ambavyo vimekwisha sambaazwa nchi nzima.
Mbali
na hayo Mwenyekiti wa NEC alitoa ufafanuzi kwa waangalizi hao wa
uchaguzi katika suala la wapiga kura kutosimama hata baada ya mita 200
katika vituo vya kupiga kura.
“Tume
iliamua kutoa tamko hilo baada ya kuona changamoto za wapiga kura na
kuamua kutoa maelekezo kuwa watu wakishapiga kura waondoke
vituoni wakaendelee na shughuli zao,lakini hata hivyo kwasasa suala
liko mahamamani lakini msimamo wa Tume ni ule ule kwani mikusanyiko
hiyo huweza kuchangia uvunjifu wa amani ila tataendelea kusikiliza
mahakama itaamua nini” aliongeza Jaji Lubuva.
Aidha
Tume imesema uchanguzi unaonekana kufuatiliwa na wananchi wengi na wito
wake kwa wananchi hao ni kwenda kupiga kura huku wakilinda amani na
utulivu wan chi A kwa kuondoka katika kituo cha kupiga kura na kwenda
kuendelea na shuguli zao na kuwataka warudi vituoni jioni kuangalia
matokeo.
Hata
hivyo tume imewataka viongozi wadini waendelee kuhubiri amani kwa
waumini wake na kuwasihi viongozi wa vyama waache kuwaambia wafuasi wao
wabaki vituoni mara baaada ya kupiga kura kwani mikusanyiko hiyo huweza
kuchangia uvunjifu wa amani.
Post a Comment