KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)
Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL unachukua fursa hii kuwaarifu abiria
wa treni ya deluxe ya Jumapili Oktoba 25, 2015 kutoka Dar es Salaam
kwenda Mwanza kuwa muda wa kuondoka umesogezwa mbele kutoka saa 2
asubuhi hadi saa 2 usiku wa siku hiyohiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo uamuzi huo umechukuliwa maalum ili kuwapa fursa
Abiria waliojiandikisha kupiga kura kutumia haki yao ya kikatiba
kikamilifu.
Utaratibu
huu utatumika pia kwa treni kwa siku hiyo zitakazokuwa zinaanza safari
zake kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam nazo zitaanza safari
hizo saa 2 usiku.
Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.
Shime kila Mtanzania ajitokeze kwenda kutumia haki yake ya kikatiba kwa kumchagua Kiongozi mwenye sera anayoiafiki.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.
Dar es Salaam,
Oktoba 21, 2015
Post a Comment