CHAMA
cha Mapinduzi CCM kimezidi kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi
katika uchaguzi mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25
baada ya kubuni mkakati mpya
wa ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia simu wananchi akiomba wampigie kura.
Ujumbe
huo unaokwenda kwa watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali humfikia
mmiliki wa simu kupitia namba +255622333333 na mara baada ya simu hiyo
kupokelewa husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania kumpigia
kura ili aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais.
Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu za kuwafikia watanzania wote bila
kujali itikadi zao na zaidi wale baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya
kusikia mambo yapi yatafanywa na mgombea huyo endapo kama atafanikiwa
kuwa rais.
Ukiacha utaratibu wa kampeni za moja kwa moja
majukwaani, mabango, mahojiano katika televisheni, hatua ya Chama cha
Mapinduzi kubuni njia ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi utawasaidia
kujiongezea kura katika uchaguzi huo unaonekana kuwa na ushindani
mkubwa.
Pengine hili ndio bao la mkono lililowahi
kusemwa kipindi cha nyuma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho
Nape Nnauye kutokana na hatua hiyo kuwa muhimu hususani wakati huu ambao
watanzania wengi wanamiliki simu za mkononi.
Kutokana
na hatua hiyo ina maana kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia mgombea
huyo akiwaomba kura mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia sauti
yake ikiomba kumchagua katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais wa
awamu ya tano wa taifa hili.
Chama cha Mapinduzi CCM kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika
kijiti kinachotarajiwa kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache
zijazo.
Post a Comment