Wahenga walisema
utakiona cha mtema kuni! Ndivyo ilivyomtokea kijana anayedaiwa ndiye
sharobaro maarufu eneo la Himo katika Jimbo la Vunjo, Kilimanjaro
aliyejitambulisha kwa jina la Steven Charles baada ya kumfanyia fujo
mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe
Magufuli katika jimbo hilo wakati akinadi sera zake.
Katika
tukio hilo Dk. Magufuli akiwa anaendelea kumwaga sera katika mkutano
huo uliohudhuriwa na umati mkubwa, Steven alidaiwa kuanzisha fujo
katikati ya umati huo na kusababisha mkutano kutawaliwa na vurugu huku
watu wakishindwa kumsikiliza mgombea huyo.
Vurugu
hizo zilipoongezeka, Dk. Magufuli alisimamisha zoezi la kunadi sera
zake na kuwaomba wanausalama kumdhibiti kijana huyo aliyekuwa akifanya
vurugu wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo.
Baada
ya kusikia amri hiyo, kundi la maafande wa FFU almaarufu Fanya Fujo
Uone lilikwenda kumchomoa Steven sehemu aliyokuwa akihamasisha vurugu na
kumbeba msobemsobe huku wamemkwida shati na kwenda kumtia kwenye
karandinga.
Shuruba
alizozipata kijana huyo ndani ya dakika kama nne zilitosha kabisa
kulinganisha kibano hicho na kilichomtoa khanga manyoya kama isemavyo
kauli ya wahenga.
Post a Comment