Gari lilokodiwa na tume ya uchaguzi ya Wilaya ya Arumeru Mashariki limezua utata baada ya kukutwa na kiasi cha fedha zaidi ya Sh 6 milioni.
Akizungumzia
sakata hilo, Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi, kata ya Imbaseny , Jefason
Mwangura ,amekiri kubeba fedha hizo kwenye gari hilo mali ya Enong’oto
na kudai kuwa zilikuwa ni za malipo ya wasaidizi wa vituoni kwa ajili
ya kujikimu.
Alisema pia pesa hizo kwa utaratibu ilikuwa ni kulipa wasaidizi vituoni ili iweze kuwasaidia kujikimu wakiwa vituoni hapo .
Hata
hivyo , Mwangura alisema Mwenyekiti wa Chadema, kata ya Imbaseny
baada ya kukamata fedha hizo alikimbia nazo kusikofahamika.
“Mimi nashangaa hela zimechukuliwa na aliyechukua amekimbia nazo ,” kama ilikuwa si halali wangezishika wasubiri polisi ,”alisema Jefason
Mgombea
ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,(chadema) Joshua Nasari
alizungumzia tukio hilo na kusema ni kosa kisheria kuzunguka na fedha
hizo kwani kisheria ilipaswa zilipwe kabla au baada ya uchaguzi.
Post a Comment