Wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura kwa nafasi ya udiwani kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.
Akiongea
na waandishi wa habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah
Malela amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa
ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.
Alisema
kuwa kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini
karatasi ambazo zimetoka Tume ya uchaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi
ya wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.
“Baada
ya kuona hali hiyo niliwasiliana na viongozi wa tume kutoa taarifa
ambao waliamua kuhairisha zoezi kwa nafasi ya udiwani tu, mpaka tena
itakapotangazwa na tume,” alsiema Malela.
Kwa upande wa rais na mbunge, zoezi liliendelea kama kawaida kwa kuwa karatasi hizo zililetwa za kutosha.
Kwa
upande wa Jimbo la Itilima Mkoani hapa Msimamizi wa uchaguzi
Alphonce Aloyce alisema zoezi lilienda salama licha ya mihuri kukwama
ingawa tatizo hilo lilipatiwa ufumbuzi mapema.
Post a Comment