Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Haji Duni
amesema kuwa wamegundua njama iliyopangwa na Chama cha Mapinduzi CCM
pamoja na Tume ya uchaguzi kwamba kura zikitoka kwenye vituo zipite
kwenye mtandao na kuziiba kwa kutumia wataalamu wao wa TEHAMA.
Ameyasema hayo mapema leo wakati wa kufunga kampeni kwa vyama
vinavyounda umoja huo zilizofanyika katika viwanja vya jangwani jijini
Dar es Salaam
Duni amesema kuwa CCM imetayarisha wataalam wawili ambao watafanya
kazi hiyo na kwamba UKAWA watajitahidi kuweka kumbukumbu iliyosahihi ya
matokeo ya kura zao zote ili kuepusha wizi unaotaka kufanywa.
Ameongeza kuwa kila wakala lazima apatiwe nyaraka ya matokeo ya kura iliyotiwa saini,
Aliwataja wataalam hao kuwa ni Mr Mkanyanga na Sesy Francis ambao
ndio wamekabidhiwa kuiba kura katika kituo cha Kurasini karibu na makao
makuu ya uhamiaji.
“Wakileta mchezo tutawaambia wananchi wakakizunguke alafu tutaona
kama hodari ni Rais Kikwete au wananchi …..Kikwete umeambiwa ukabidhi
nchi kama ulivyopewa kwa amani na akuna Jeshi linaloweza kupiagana na
umma,”amesema Duni.
Post a Comment