MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa amesema wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha Dodoma watapiga kura kwenye maeneo waliyojiandikisha.
Alisema hayo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho.
Baadhi ya vyuo vya mkoa huo ni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo
Kikuu cha St. John, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Serikali
za Mitaa, Chuo cha Mipango na Chuo cha Madini.
Akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari ni wapi wanafunzi wa
vyuo vikuu watapiga kura kutokana na utata uliopo kuwa si wakazi wa mkoa
wa Dodoma na kwamba kuna taarifa kuwa watasafirishwa kwa mabasi ili kufika
Dodoma kupiga kura.
Gallawa alisema tume ilitaka watu wajiandikishe kituo chochote lakini
kuna baadhi ya vituo viliandikisha watu wengi wa nje kuliko wakazi wa
eneo husika, hali inayozua maswali mengi kuwa wakazi wa pale
watachaguliwa diwani.
“Mfano utakuta kata ina watu 1,700 ambao si wakazi waliojiandikisha,
wanafikia 5,000 lakini ukiangalia kwa undani suala hili utaona hali
halisi ilivyo,” alisema.
Katika hatua nyingine, wasimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya zote saba
za mkoa wa Dodoma wameshapokea fedha za kuendesha uchaguzi mkuu na
mafunzo kwa watendaji watakaoshiriki katika uchaguzi yanahitimishwa
kwenye wilaya zote.
Waliojiandikisha ni wananchi 1,053,136 kuwa wapiga kura sawa na
asilimia 102.7 ya lengo, ambapo lengo lilikuwa ni kuandikisha wapigakura
1,025,084.
1 comments:
Hii habri inasikitisha sana na Mkuu wa mkoa hafai Tanzania yetu ni moja kwanini anaongea hivyo katiba ya Tanzania haisemi eti wapi mtu anatakiwa kuishi... Yeye kwao Dodoma...!!!
ReplyPost a Comment