Sehemu
ya Kinu cha Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini Dar es Salaam
ambako dawa za kulevya zimeteketezwa jana chini ya uangalizi mkali .
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzichoma moto katika
kinu hicho Jaji wa Mahakama Kuu Edison Mkasimongwa alizitaja aina ya
dawa hizo kuwa ni Heroine mifuko 179 na Cocaine mifuko 81 zenye thamani
ya Shilingi Bilioni tano ambapo zilikuwa na Gram 175,000 ambazo zilikamatwa miaka kadhaa Mbezi Jogoo jijini Dar.
Jaji
wa Mahakama Kuu Edison Mkasimongwa(kulia) akihakiki sehemu ya kinu
cha kuchomea madawa hayo ya kulevya uku akisindikizwa na Mkurugenzi wa
Mashtaka Biswalo Mganga(kushoto) katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini Dar es Salaam
Hii ndio sehemu ya mfuniko wa kinu kilichotumika kuchomea dawa za kulevya
Askari
wakifungua maboksi yaliyokuwa yamebeba dawa hizo za kulevya kwa ajili
ya kuziteketeza katika kinu cha kiwanda cha Saruji hapa jijini Dar.
Jaji
wa Mahakama Kuu Edson Masimongwa(kushoto) akifungua moja ya boksi
lililobeba dawa za kulevya kwa ajili ya kuhakiki pamoja na kuziteketeza
dawa hizo
Askari akizihakiki dawa za kulevya kwa kuzihesabu ili kuziteketeza ambapo zoezi hili lilifanyika katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini Dar es Salaam jana mchana
Sehemu ya Dawa za kulevya zilizoteketezwa jana katika Kiwanda
Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini Dar es Salaam uku zikisimamiwa na
majaji wa mahakama Kuu, jeshi la Polisi pamoja na mamlaka ya kudhibiti
Dawa za kulevya hapa nchini
Mfanyakazi
kutoka kampuni tya Saruji ya Twiga akiziteketeza dawa uku akisimamiwa
na jeshi lapolisi, maofisa wa mahakama pamoja na viongozi wa kudhibiti
Dawa za kulevya hapa nchini hapo jana katika kiwanda hicho
Maofisa
kutika mahakama pamoja na maofisa kutika mamlaka ya udhibiti wa dawa za
kulevya wakifuatilia tukio la kuteketeza dawa hizo
Post a Comment