MAYASA MARIWATA NA BONIPHACE NGUMIJE
MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwandani wake Ally Salehe
Kiba, wamethibitisha kuwa wana maelewano mazuri (picha zinaiva) baada ya
mwishoni mwa wiki kuonekana pamoja katika bonanza maalum la wanafunzi,
lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Jangwani, jijini Dar
es Salaam.
Tukio hilo lililojulikana kama Kidoti Bonanza liliandaliwa maalum kwa
ajili ya kuthamini vipaji vya wanafunzi na ambalo lilihudhuriwa na
madenti wa shule mbalimbali ambao pia walipata burudani kutoka kwa
wasanii na makundi tofauti.
Jokate alikuwa jukwaani pamoja na msanii anayetamba na kibao cha Ni
Yule, Hellen George ‘Ruby’ ambaye alishika kipaza sauti na kuwauliza
madenti hao kama wanafahamu mtu aliyeimbwa na Kidoti katika kibao chake
cha Leoleo ambao wote kwa pamoja walijibu kuwa mtu huyo ni Ali Kiba.
....Wakiwa stejini.
“Hivi nataka niwaulize, mnajua ile nyimbo Jokate aliposema anamvizia
anapokatisha akienda mpirani alikuwa kamlenga nani,” aliuliza Ruby
ambaye alikuwa ‘akimkata’ jicho Jokate aliyekuwa akiangua kicheko muda
wote.
Muda mchache baadaye, Ally Kiba aliwasili eneo hilo akiwa ameongozana
na dada yake Zabibu na alipokaribia jukwaani, Jokate alimkimbilia na
kumkaribisha kwa busu na baadaye kukumbatiana bila kujali macho kodo ya
madenti.
Kama hiyo haitoshi, mkali huyo wa Bongo Fleva alipopanda jukwaani
kutumbuiza kwa sapraizi, watu walimgomea na kutaka ampandishe Jokate
acheze naye na kujikuta akifanya hivyo, japo mwanadada huyo alionekana
kuona aibu kucheza na mwandani wake huyo, wakabaki kuangaliana jambo
lililozua shangwe na kuwalazimu kucheza Wimbo wa Chekecha-Cheketua baada
ya Kiba kumlazimisha mlimbwende huyo acheze.
Jokate
alipoulizwa na paparazi wetu aliishia kucheka na kuomba aachwe kwa muda
huo kwa kuwa alikuwa `bize’, lakini ‘King Kiba’ alisema uwepo wake eneo
hilo ni jambo linalojionyesha wazi kwani hakuna siri tena.
“Sipendi kuyaongelea hayo mambo, lakini hiyo imeshakuwa gumzo la jiji
na nyinyi kama wanahabari kila kitu kinajionesha, kama kusoma huwezi
basi hata picha huoni? Kilichonileta hapa ni kumsapoti Jokate sababu
kitu anachokifanya ni kizuri na nitamuunga mkono mwanzo mwisho katika
kila jambo.”
Post a Comment