Kutoka
Kushoto - Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava,
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Nishati na Madini (Uganda), Dkt. Fred
Kabagambe Kaliisa na Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Ndg. Adewale
Fayemi wakipongezana baada ya kutia saini Hati ya Makubaliano (MoU)
baina ya Serikali ya Uganda na Tanzania juu ya utekelezaji wa mradi wa
bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda (Kabaale) mpaka bandari
ya Tanga (Tanzania).
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC)
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda, TPDC na Total
E&P Uganda wametia saini Hati ya Makubaliano juu ya utekelezaji wa
mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia Tanzania.
Hati hii
ya Makubaliano inafungua fursa kwa Serikali hizi mbili kufanya kazi kwa
pamoja kuangalia uwezekano wa kuendeleza mradi wa kusafirisha mafuta
ghafi kutoka Kabaale Uganda kupitia Tanzania mpaka bandari ya Tanga.
Makubaliano haya pia yanatambua faida zaidi zitakazopatikana kwa
Tanzania na Uganda ambazo ni zaidi ya utekelezaji wa mradi huu. Vilevile
makubaliano haya yanatoa muongozo kwa pande zote zinazohusika kuendelea
kufanya kazi kwa pamoja kuboresha tafiti zilizo kwisha fanyika juu ya
njia ya Tanga.
Akiongea
baada ya kusaini hati hiyo, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na
Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alisema “Tanzania na Uganda wana historia
ndefu ya ushirikiano na mradi huu utazidi kuboresha ushirika kati ya
nchi hizi”. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James
Mataragio aliongeza kuwa, TPDC ina uzoefu wa muda mrefu katika ujenzi,
uendeshaji na utunzaji wa bomba na hivyo uzoefu huu utasaidia sana
katika utekelezaji wa mradi huu. Wiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania alifungua rasmi mradi wa bomba la gesi la kilometa 542
kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam unaomilikiwa na kuendeshwa na TPDC.
Imetolewa na;
Mkurugenzi Mtendaji,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,
S.L.P 2774,
Dar-es-Salaam.
Tanzania
www.tpdc-tz.com (
Mkurugenzi Mtendaji,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,
S.L.P 2774,
Dar-es-Salaam.
Tanzania
www.tpdc-tz.com (
Post a Comment